HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 17, 2012

WAMACHINGA JIJINI MBEYA WANAVYOENDELEA KUJIDAI KATIKA MAENEO YASIYO RASMI

Ofisi ya TRA mkoa  wa Mbeya uzio wake ukiwa umepambwa na mataulo ya yanayouzwa na wamachinga huku mamlaka husika zikiwatizama tu wamachinga hao bila ya kuwachukulia hatua yeyote
Barabara ya kuingia katikati ya jiji la mbeya pembeni ya jengo la TRA mkoa wa Mbeya wamachinga wapo huru kabisa huku waenda kwa miguu wakipita barabara ya magari kana kwamba hawana njia yao ya kupita mambo hayo ya jiji la mbeya sijui nani anaehusika kwa hili
Kutokea eneo hili ni hatua chache sana kufika katika ofisi kuu za halmashauri ya jiji la mbeya na ni njia kuu ya kupita viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika barabara hii je haya ni mapambo?
Ofisi za TRA mkoa wa Mbeya zikiwa zimezungukwa na badhaa mbalimbali za wamachinga hao
Cha ajabu mgambo wa jiji wanahangaika na vijana waosha magari mjini huku wamachinga wakiwaacha wakichafua mji kwa kupanga vitu vyao kiholela tena katikati ya mji na ofisi kuu za serikali na taasisi kubwa za kibenki.Picha na Mbeya Yetu Blog.

2 comments:

  1. Kwani hawa wanamuibia mtu?, wanajitafutia rizki kihalali wewe inakuuma nini, acha kijicho,mbona mafisadi hamuwasemi wakati mnawajua. just mind your business.

    ReplyDelete
  2. Fanyeni biashara Watz wangu ilimradi hamjaiba cha mtu. Tena hata ikiwezekana nendeni pale mlangoni mwa wabunge mkawauzie. Msikubali ng'o

    ReplyDelete

Post Bottom Ad