HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 13, 2012

ujumbe wa IMF waongea na waandishi wa habari jijini Dar leo

Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum (kushoto) kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishwa na ukame mwaka 2011 kulia ni Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
aadhi ya wajumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mjumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika ambaye jina lake halikupatikana mara moja akimrekodi kwa kutumia simu ya mkononi Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum (hayupo pichani) wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad