Niko Dar es Salaam. Hili ni Jiji la lawama kwa maana zote. Kila unayekutana naye analalamika. Mtu wa kwanza kukutana nae kwenye ofisi moja ananiuliza; " Mbona huonekani mjini!" Kana kwamba watu wote tunaishi mjini na kuwa lazima tuonekane!Haah....!!
Naam, kila mmoja anatoa lawama. Hata kunguru wa Dar siku hizi wanatoa milio ya kulalamika! Wala haipendezi masikioni. Masikini, Dar ilikuwa na ndege wengi wazuri na wenye sauti za kuvutia, wamekimbilia wapi? Naam, na leo Dar joto ni kali na jua linawaka kama tumekaribia kiyama. Well, all in all, Dar is the City I'm born, and still has it's charms! Haki ya Mungu!
No comments:
Post a Comment