HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 13, 2012

Kifaa Kipya cha Kuzima Moto chazinduliwa Jijini Dar leo

 Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw.  Mbarak Abdulwakil pamoja na Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi inayotengeneza vifaa vya kuzimia moto vyenye teknolojia ya kisasa vinavyoitwa DSPA 5, wakikiandaa kifaa hicho kwa ajili ya kukirusha ndani ya kontena lililowashwa moto, ili kufunga mlango na kuruhusu kifaa hicho kufungua gesi ya Oxgen baada ya sekunde sita tayari  kuzima moto huo ndani ya kontena hilo, tukio hilo lilikuwa ni uzinduzi wa vifaa hivyo hapa nchini, uliofanyika katika viwanja vya Kikosi cha kuzima moto Fire jijini Dar es salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil kulia  akipokea moja ya vifaa hivyo DSPA 5 kutoka kwa  Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya  Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini , wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa kikosi cha Zimamoto  Kamanda Pius Nyambacha na anayefuatia ni Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi. 
 Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi,Frans Vogelzangs akimwelekeza katibu mkuu Mbarak Abdulwakil katikati jinsi ya kuuweka ufunguo wa kifaa hicho kabla ya kukirusha ndani ya kontena lenye moto, Kushoto ni Damian George Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi,Frans Vogelzangs akiwaelezea wageni waalikwa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi.
 Askari wa Kikosi cha kuzima mto wakiwa tayari kwa kuzima masalia madogo madogo ya moto baada ya kifaa hicho kufanya kazi yake kikamilifu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil pamoja na viongozi wa kampuni hiyo na wakuu wa kikosi cha kuzima moto wakishuhudia moshi mkubwa ukitoka kwenye kontena hilo baada ya kifaa hicho kuanza kazi yake ya kuzima moto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil kushoto akipokelewa na  Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya  Your Solution Limited na makamanda wa kikosi cha Zima moto, mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio tayari kwa uzinduzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad