Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo ambayo nimefanikiwa kuongeza namba moja katika umri wangu,kwani bila yeye ni kwamba hakuna kitu chochote kinachoendelea.
pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwepo wazazi) kwa kunilea na kukikuza katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.
pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu,Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote.
Katika siku hii Muhimu,sipo peke yangu,kwani ni wengi pia tumezaliwa siku kama ya leo wakiwemo wadau hawa wanaoonekana kwenye picha hicho hapo chini.
SASA TUNAZISUBIRIA HIZO ZAWADI ZETU KWA HAMU.
SASA TUNAZISUBIRIA HIZO ZAWADI ZETU KWA HAMU.
Mdau Dj LUKE Mzee wa Vijimambo.
Khalifa Ilunga a.k.a CPWAA.
Farha Sultan.
hebi besde kijana... kua tukutume!
ReplyDeletemdau from Orange