Nikiwa sina hili wala lile huku nikitafakari ni namna gani nitakavyo siku yangu hii muhimu katika maisha yangu itakavyomalizika,ghafla nikaona kilongalonga changu kinawaka waka (maana siwekagi mlio),nikakichukua na kuangalia ni nani aliekuwa akinitwangia,nikabaini kuwa rafiki yangu ndie aliekuwa akinitwangia na kuniuliza mahali nilipo?nami kwa unyoooonge nikajibu nipo Home.akanambia kuwa kuna jambo la muhimu sana nataka kuchonga nawe kuhusu mipango ya ile kazi (ambayo aliniomba nimsaidie kuifanya),sasa naweza kukuonana nawe mida hii??nikauchuna kidogo na kumwambia nimechoka sana leo hivyo naomba tufanye kesho,maana leo sijisikii kwenda mahali popote.akanisisitiza tena kuwa ni muhimu sana na nilazima iwe leo ili kesho tuyafanye matekelezo yake,ndipo nikamuliza mahali alipo (kwani alikuwa nyumbani kwao ambako si mbali sana na kwangu) nami tarrrrtiiibu nikaanza kujivuta kuelekea mahala hapo.ile kufika tu nikaona kama vile umeme umekatika,hivyo nikanyanyua simu yangu na kumpigia yule aliehitaji kuonana nami na alipokea na kuniambia naja hapo sasa hivi,kweli muda si mrefu alifika na ndipo nikamuuliza vipi mbona giza kwenu leo,akanambia umeme uliisha na ndio nilikuwa nimetoka kununua,na akaweka ule umeme mitani.ile kuwasha tu .ndipo nikakutana na bonge moja la Sapraizz ambapo nilibaki kushangaa tu kwani niliona watu ambao hata sikutaraji kuwaona hapo muda huo huku nikiona bonge la JIKEKI pale mezani kwao likiwa na jina langu.yaani hata sikuamini kilichotokea.Kiukwaeli nawashukuru sana wale woote walioniandahii sapraizz na kwa moyo wao mzuri walionionyesha na kuwaombea kwa mungu awajaalie zaidi na zaidi.Daahhh..... sijui nlieeee??
Saturday, March 3, 2012

Home
Unlabelled
Hepi Besdei ya Kuzaliwa Kwangu leo ilivyoadhimishwa
Hepi Besdei ya Kuzaliwa Kwangu leo ilivyoadhimishwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
sitaki kuamini nimekosa jikeki..
ReplyDeletehepi besidei
ReplyDeleteHONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KEKI INAONEKANA TAMU KWELI.
ReplyDeleteHappy Birthday.....kila lakheri kwa yote na maisha marefu!
ReplyDelete