Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania,Sam Ellangallor akiongea na wafanyakazi wa Airtel wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy iliyofanyika leo katika Makao makuu ya Airtel Morocco.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania,Adriana Lyamba akiongeaa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel,Perece Kiringiti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Perece Kiringiti akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja,Adriana Lyamba.
Keki maalumu ya uzinduzi wa programme ya Airtel Service Academy.
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi iliyofanyika katika Makao makuu ya Airtel Morocco.
Airtel Tanzania, mtandao unaoongoza kwa gharama nafuu na wenye wigo mkubwa Tanzania leo umezindua programu ya kuwawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora Tanzania.
Hii inakuja baada ya ya uzinduzi mzuri wa chuo cha masoko kilichozinduliwa mwezi wa kumi mwaka jana inayojulikana kama " Airtel Centum Sales University (ACSU)" Akiongea katika uzinduzi wa programu hii ya mafunzo kwa timu zinazotoa huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel ,Mkurugenzi wa Airtel Tanzania bwana Sam Elangalloor alisema,"Leo tunazindua rasmi mafunzo ya huduma kwa wateja Tanzania inayoashiria dhamira yetu katika kuleta mabadiliko na kuwaopa wateja wetu huduma bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.lengo letu ni kuhakikisha tunatoa huduma ambazo zinazidi matarajio ya wateja wetu na kudumisha mahusiano ya muda mrefu.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa uteja, Adriana Lyamba aliongeza kwa kusema, "mafunzo haya ni muendelezo wa kuonyesha ni kwa jinzi gani kampuni na nembo yetu inajali wateja wake.Katika siku 365 zijazo wafanyakazi wa Airtel katika kityengo cha huduma kwa wateja watajifunza mbinu za kitabia na zile za kikazi katika kutoa ufanisi zaidi na kuwaongezea ujuzi zaidi.
Leo Tanzania zaidi ya wafanyazi 99 wa kitengo cha huduma kwa wateja wataanza mafunzo haya ya huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel makao makuu.
Programu hii ya Airtel service Academy inatolewa na kampuni ya ukufunzi ijulikanayo kama Centum learning na itahakikisha watoa huduma wa Airtel wanakua bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment