Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisamiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,Michael Kamuhanda wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa mjini Songea mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu (kushoto) akikabidhi taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Meneja wa wakala wahifadhi ya taifa ya chakula kituo cha Songea,Morgan Mwaipyana (kushoto) akimkabidhi Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal taarifa ya kituo hicho ambacho hadi sasa kinakabiliwa na upungufu wa fedha za kununulia mahindi ya wakulima ambayo bado yapo majumbani kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.
Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal akizungumza na wakazi wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma katika viwanja vya manispaa ya Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (hayupo pichani) katika viwanja vya ikulu mjini Songea.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu (wa pili kushoto) akimuonesha Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (katikati) moja ya maghala ya kuhifadhia mahindi katika kituo cha wakala wa hifadhi ya chakula ya taifa kituo cha Songea.
Meneja wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula kituo cha Songea,Morgan Mwaipyana (kulia) akimueleza jambo Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (kulia) juu ya kukosekana kwa maghala ya kutosha ya kuhifadhi mahindi ambapo hadi sasa yaliyopo yanauwezo wa kuhifadhi tani 26 huku kiasi walichonacho ni zaidi ya tani 40.PICHA NA MUHIDIN AMRI .
No comments:
Post a Comment