Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni (mstaafu) Chiku Gallawa akitazama moja ya mifuko ya kufungashia bidhaa inayotengenezwa na kiwanda cha Pee Pee Tanzania Limited (PPTL) kilichopo Jijini Tanga, mfuko huo ni wa kiwanda cha Simba Cement cha Tanga. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa PPTL Bw. Jonathan Lane (kushoto kwa RC), anayemfuata ni Bw. Chetan Taishete (mdhibiti wa fedha PPTL), kulia kwa RC ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi na Bw. Dominick Mtemangwa Meneja wa kiwanda cha PPTL.
Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha PPTL, Bw. Lane akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mh. Chiku Gallawa alipotembelea kiwanda hicho kuona uzalishaji ambapo hapo alikuta mifuko mingi ya viwanda mbalimbali hapa nchini kama kulia mifuko ya kiwanda cha saruji Mbeya.
Mkuu wa mkoa akitembelea kiwanda cha Arthi-River kuona namna wanavyoendelea na ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kukamilika kwake kutaufanya mkoa wa Tanga uwe na viwanda viwili vinavyozalisha saruji.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kiwanda cha saruji kipya cha Arhi-River kitakachozalisha saruji chapa Rhino-Cement. Kiwanda hicho bado hakijakamilika licha ya ungozi wa kiwanda kumwahidi Rais Jakaya Kikwete alipofungua kiwanda hicho mwaka 2010 kwamba kitamalizika katika kipindi cha miezi 24 lakini hadi sasa ujenzi wake bado haujakamilika ni kiasi cha asilimia 54 kimekamilika na kinatarajiwa kukamilika mapema mwakani.
Na Mashaka Mhando,Tanga
WAWEKEZAJI wa sekta ya viwanda mkoani Tanga, wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa vijana wenye utaalamu wa kuendesha mashine mbalimbali za viwanda vyao.
Akizungumza mara baada ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Pee Pee Tanzania Limited (PPTL) Bw. Jonathan Lane alisema kuwa kiwanda chao chenye wafanyakazi wapatao 1,000 wengi wao wakiwa akina mama, kimekuwa kikikabiliwa na wataalamu waendesha mitambo 'Mafundi mchundo' kutokana na kukosekana hapa nchini.
Alisema vijana wengi wanaomaliza elimu ya juu ikiwemo vyuo vikuu wanapofika kufanya usaili katika kiwanda hicho, kwanza wamekuwa na mapungufu makubwa ya lugha ya mawasiliano ikiwemo udhoefu wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho hivyo kushindwa kuwachukua.
"Hapa kiwanda tunakosa wataalamu kutoka hapa Tanzania, tunapowaita vijana wanaomaliza vyuo vikuu kwenye Interview (usaili) wanakuwa lugha tu inakuwa shida na jingine hawawezi kuendesha mashine hizi tunazotumia inakuwa shida kuwaajiri tuna lazimika kuchukua wataalamu kutoka nje kama Kenya," alisema Bw. Lane.
Akichangia suala hilo Meneja wa kiwanda hicho Bw. Dominick Mtemangwa alisema suala kubwa linalosababisha wahitimu wengi wa vyuo vikuu kushindwa kuwa na utaalamu wa kuendesha mashine ni kutoka na kusoma kwa nadharia tofauti na miaka yao ambayo kabla ya kwenda chuo kikuu walikuwa wakipitia katika vyuo vya FTC ambako huko hukutana na mashine mbalimbali zinazowapa urahisi wa kufanya vizuri kwenye mitihani na kivitendo
Halkadhalika Mkuu wa mkoa huyo, alipofika kutembelea kiwanda cha Arthi-River Meneja mradi wa kiwanda hicho Bw. Rajesh Vyas alisema wanatangaza nafasi za vijana wa mkoani Tanga wenye ujuzi wa kazi mablimbali katika kiwanda chao, lakini hakuna anayejitokeza na wakijitokeza wanakuwa hawana ujuzi hivyo kupata wakati mkumu wa kukamilika mapema kiwanda hicho kama walivyoaahidi.
Alisema pamoja na suala hilo tayari wamewafundiusha vijana wapatao 30 kwa fani mbalimbali katika kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unakwenda sambasamba na kiwanda chao kingine kilichopo wilayani Mkuranga, Pwani kitakachokuwa na ukubwa sawa na cha tanga.
Akizungumza suala hilo, Mkuu wa mkoa alisema kuwa kwa mpango wa haraka atakutana na Mkuu wa chuo cha VETA mkoani hapa, kuangalia kwa haraka fani ambazo zinatolewa hapo ili kuwawezesha vijana watakaochukua mafunzo hapo waweze kupata ajira katika viwanda hivyo.
Pamoja na kueleza hayo pia, aliwapongeza viongozi wa viwanda vyote viwili kwa kutambua suala uhifadhi wa mazingira katika viwanda vyao kutokana na kemikali wanazotumia na hasa suala la uchimbaji wa mawe na hivyo mashimo yaweza kubaki yakaleta athari za kimazingira lakini kiwanda cha Arthi-River mara baada ya kuchimba mawe hayo wamekuwa wakiyatunza mashimo mengine kwa ajili ya kuhifadhi maji.
No comments:
Post a Comment