Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za siku ya Sheria,Zanzibar,(kulia) ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Abubakar Khamis,na Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fakih Jundu,(kushoto) ambapo "kauli mbiu kuga vita Rushwa katika utowaji wa haki" ,sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Ali Abdalla Ali,(kulia) Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis,(kushoto)Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fakih Jundu,na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Abubakar Khamis, wakiwa wamesimama wimbo wa taifa ukipigwa na kikundi cha polisi Brass Band katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika Victoria Gaden Mjini Unguja.
Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Zanzibar Mhe.Ibrahim Mzee,akitoa hotuba yake na kumkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman,wakati wa Sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.
Baadhi ya viongozi wa Dini na Majaji wa wilaya za Unguja waliohudhuria katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar,huko katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa sherehe hizo.
Baadhi ya wananchi na viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za siku ya Sheria Zanzibar,ambvapo kila ifikapo Tr 7 Feb ya kila mwaka huadhimishwa kwa kusherehekea siku hiyo,hafla ya sherehe zilizofanyika katika, katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana na Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,(katikati) na Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Fakih Jundu,alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za siku ya Sheria,Zanzibar.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,akiongoza maandamano ya majaji na wanasheria wa serikali na wakujitegemea wakati wa Sherehe za Siku ya Sheria,ambapo kauli Mbiu ya mwaka huu "Kupiga vita rushwa katika utowaji wa haki",sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
No comments:
Post a Comment