HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2012

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA KUFANYIKA 25 FEB. 2012

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome, unayofuraha kuwajulisha wanajumuiya wake wote kuwa siku ya jumamosi tarehe 25 februari 2012 kuanzia saa nane mchana, kutakuwa na mkutano utakaoambatana na uchaguzi wa viongozi wapya wa Jumuiya ya Watanzania Rome.

Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome kwenye mtaa wa Via Cortina d'anpezzo 185. 

Wanajumuiya hai wote mnaombwa muwasiliane na katibu ndugu Andrew Chole Mhella ili muweze kupata utaratibu nzima wa mkutano. Mnaweza kumpata katibu kwa e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it au kwa simu namba 3479094800. 

Kwa wale ambao wanapenda kuwasilisha majina yao kwaajiri ya kugombea nafasi hizi mnaombwa mtume majina yenu yakiambatanishwa na nafasi ambayo mnataka kugombea kupitia e-mail ya jumuiya hapo juu. Nafasi ni hizi MWENYEKITI, MWENYEKITI MSAIDIZI, KATIBU, KATIBU MSAIDIZI, MWEHA HAZINA NA NAFASI MBILI ZA WAJUMBE.

Uchaguzi utaendeshwa kwa kufuata kanuni za katiba.

Kwa maelezo zaidi temebeleeni hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad