Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akifunua pazia kuonesha jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa mtambo wa nne wa usafishaji maji yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama kwa matumizi ya binadamu katika hafla iliyofanyika katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha,mwishoni mwa wiki.Anayeshuhudia uzinduzi wa mtambo huo uliogharimu sh. bilioni 3.6, ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche.
Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk. Cyril Chami, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akisalimiana na viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa nne wa usafishaji maji yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama kwa matumizi ya binadamu katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, mwishoni mwa wiki.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL, Gavin van Wijk, Meneja wa Kiwanda TBL Arusha,Bert Grobbelaar na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Robin Goetzsche. Wa pili kulia ni Waziri wa viwanda na Biashara,Dk. Cyril Chami.
Msimamizi wa Mtambo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa kusafisha maji taka kuwa salama kwa matumizi ya binadamu, Said Lwambo kutoka Kampuni ya Talbot & Talbot, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami (wa tatu kushoto) kuhusu usalama wa maji hayo wakati wa uzinduzi wa mtambo huo uliogharimu sh. bil 3.6 ambao ulifanyika hivi karibuni katika kiwanda cha TBL Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto), akifurahia jambo walipokuwa wakitembelea mtambo huo.
No comments:
Post a Comment