HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 15, 2012

SOKO LISILO RASMI ENEO LA UBUNGO MATAA LINAVYOZIDI KUKUA KWA KASI SIKU HADI SIKU

Wafanyabiashara wadogo wadogo wajulikanao kama wamachinga wakiwa wamepanga bidhaa zao katika kituo cha kidogo cha mabasi Ubungo kama unavyowaona mwenyewe, kwasasa biashara katika eneo hilo imeshamili sana mpaka wahusika wamejisahau kabisa sijui serikali inafanyaje kuhusu watu hawa???
kila kitu kinapatikana hakuna haja ya kwenda sokoni ama kwenye maduka.

Hali ya Bara bara ya Morogoro Road eneo la Ubungo mataa lipo katika hali ya hatari sana, hasa kutokana na kasi ya wafanya biashara ndogo ndogo ,maarufu kama wamachinga wanavyoongezeka kwa kasi katika eneo hilo, ni jambo la kushangaza sana kuona hali hii inavyoachwa kana kwamba wahusika hawaioni, tunapenda kuwaasa kwa mara nyingine tena Serikali jaribuni kuliangalia hili, wafanya biashara hawa wanafanya biashara katika mazingira ya hatari sana na yasiyo rasmi.Picha na Mdau Henry Henry.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad