HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 9, 2012

Rais Kikwete akutana na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Johnnie Carson na ujumbe wake leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. Johhnie Carlson na Ujumbe wake leo mara baada ya kuzungumza nao
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. Johhnie Carlson na Balozi wa Marekani Nchini,Bw. Alfonso Lenhardt walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Ujumbe wa wafanyabiashara wa Marekani katika sekta ya nishati ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Johnnie Carson umekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete hapo Februari 9 na kuwa na majadiliano kuhusu sekta ya nishati nchini Tanzania na fursa mbalimbali za uwekezaji kwa makampuni ya nishati kutoka Marekani. 

Naibu Waziri Carson na ujumbe wake waliwasili jijini Dar es Salaam hapo Februari 8 kama sehemu ya ziara ya nchi nne zikiwemo Msumbiji, Nigeria na Ghana ili kuona fursa za uwekezaji hususan katika miradi ya uzalishaji umeme. Ujumbe huu umedhaminiwa pia na Baraza la Wafanyabiashara wa Marekani kwa Afrika (The Corporate Council on Africa). 

Ziara ya ujumbe huu inathibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Marekani ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Tanzania wakati huo huo ikitangaza fursa nyingi zilizopo hapa nchini.
Ujumbe wa Naibu Waziri Carson unajumuisha wawakilishi wa makampuni ya Anadarko Petroleum, Caterpillar, Chevron, Energy International, General Electric, Pike Enterprises, Strategic Urban Development Alliance LLC, Symbion, na Zanbato Group. 

Wajumbe wengine wanaoiwakilisha Serikali ya Marekani ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa U.S. Export-Import Bank, Bi. Wanda Felton na viongozi wa Idara ya Rasilimali za Nishati ya Marekani.

Tarehe 9 Februari, ujumbe huu ulishiriki pia katika majadiliano na maafisa wa sekta ya Nishati wa serikali ya Tanzania na wa sekta binafsi yaliyofanyika katika hoteli ya Serena. Aidha ujumbe unatarajiwa kukutana na Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja, Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO William Mhando. Hapo tarehe 10 Februari, ujumbe wa Naibu Waziri Carson utatembelea Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) ambako watakuwa na majadiliano na wawakilishi wa kituo hicho, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). 

Siku hiyo hiyo ujumbe huu utashiriki katika majadiliano na chakula cha mchana na wawakilishi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Kimarekani wafanyaobiashara hapa Tanzania (American Chamber of Commerce), Baraza la Taifa la Biashara, Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake siku hiyo ya tarehe 9 Februari, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso E. Lenhardt alisema, "Tanzania ni nchi iliyojaliwa utajiri mkubwa wa maliasili na yenye fursa nyingi, hususan katika suala la nishati.

Huu ni wakati sasa wa kuvutia wawekezaji wa nje ili waungane na Watanzania na Makampuni ya Kimarekani yameonyesha nia thabiti ya kufanya biashara barani Afrika," alisema Balozi Lenhardt na kuongeza kuwa; "Sekta binafsi ni ufunguo wa kufungua fursa nyingi zitakazowezesha ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad