HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 15, 2012

MAKAMPUNI 100 KUSHIRIKI MAONYESHO YA KILIMO MKOANI ARUSHA

Makampuni 100 ya kilimo na nafaka kutoka nchi mbalimbali barani Afrika , yanatarajiwa kushiriki maonyesho ya kilimo na biashara yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha yatakazoshirikisha nchi kumi za Afrika ambazo ni wanachama wa baraza la nafaka la kanda ya Afrika Mashariki(EAGC).

Aidha maonyesho hayo yatalenga zaidi kutoa mafunzo kwa wakulima ,kuhusu kilimo ,biashara na kuweza kuonyesha ni jinsi gani wakulima hao wataweza kunufaika zaidi na mazao yao na jinsi ya kuweza kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo ,Gerald Masika aliyasema hayo katika uzinduzi wa maonyesho ya kilimo biashara yatakayofanyika jijini Arusha,

Masika aliongeza kuwa maonyesho hayo yanaandaliwa na EAGC kwa kushirikiana na kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian (SARI)kilichopo Ngaramtoni ya chini jijini Arusha na yatafanyika katika kituo hicho cha utafiti.

Alisema kuwa, maandalizi ya maonyesho hayo yanatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za kimarekani 80,000 hadi 90,000 ambapo mkulima amepewa kipaumbele zaidi kushiriki kikamilifu kutokana na umuhimu wa biashara ya kilimo na mazao.

Alifafanu kuwa, maonyesho hayo pia yatasaidia kupata utatuzi wa changamoto inayowakabili wakulima ikiwa ni pamoja na kukabilina na mbegu feki ambazo zimekuwa zikiingizwa kwenye mzunguko wa biashara za mbegu kwa mawakala wa pembejeo.

Aidha aliongeza kuwa wakulima nchini watajifunza njia mojawapo ya kukabiliana na soko la am,zao kufutaia serikali kuzuia zoezi la uvushwaji wa mazao mbalimbali hususani mahindi nje ya nchi kwani changamoto hiyo imewafanya wakulima wakate tamaa ya kulima na wengine kushia kupata kupata hasara.

Naye Mkurugenzi wa EAGC nchini , David Tuhoye aliwataka wakulima nchini kujitokeza kwa wingi katika kushiriki maonyesho hayo ili waweze kukutana na wenzao wa kutoka nchi mbalimbali na kubadilishana uzoefu.

Aidha alisema kuwa, kwa sasa wakulima kwa hapa nchini wanakabiliwa na changamoto kutokana na uuzawaji wa mahindi kutokana na serikali kupiga marufuku uvushwaji wa mahindi nje ya nchi hali ambayo imesababisha mahindi mengi kubakia kwenye maghala .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad