Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiongea wakati wa Sherehe za kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji iliyoadhimishwa jana mjini songea.Kushoto ni Kkatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi na Kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanal Mstaafu Joseph Simbakalia akiongea na wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji yaliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini humo.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi. Maimuna Tarishi na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi akiongea na wakazi wa manispaa ya songea kwenye maadhimisho ya kumbukmbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini songea jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu na kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiweka ngao na mkuki katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini songea.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi,Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoani Ruvuma,Alhaji Mustafa Songambele na Mkuu wa Zamani wa Mkoa wa Ruvuma,Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo wakiinua mikono juu ikiwa ni ishara ya kuomba dua kwa Mashujaa wa Vita ya Majimaji wakati wa maadhimisho ya Mashujaa hao mjini songea jana.
Baadhi ya wazee wa kabila la wangoni wakiwa wamevaa mavazi mfano wa yaliyokuwa yakivaliwa na machifu wa kabila hilo wakati wa ukoloni kabla ya vita vya majimaji kwenye mahadhimisho ya sherehe za kumbukumbu za nmashujaa hao jana mjini songea.Picha na Muhidin Amri.
No comments:
Post a Comment