Afisa mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla kukabidhi zawadi ya pesa taslimu kwa washindi wa wiki ya kwanza wa promosheni ya Nani Mkali,makabidhiano hayo yamefanyika makao makuu ya Kampuni ya Airtel Morocoo Jijini Dar-es-salaam, wakiwa katika picha ya pamoja ni washindi wa kutoka mkoa wa Dar es Saalam kutoka kushoto wa kwanza ni Dr.Hetal Anthan, akifatiwa na Bw Albogast Oiso na Bw Daniel Mshana.
Afisa mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akimpongeza mmoja wa washindi wa shindano la Nani Mkali Bw Daniel Mshana baada ya kusaini fomu ya kuthibitisha ushindi baada ya kujishindia pesa taslimu milioni moja katika hafla iliyofanyika makaomakuu ya Kampuni ya Airtel, wa pili kushoto ni washindi wengine ambao ni Bw Albogast Oiso akifatiwa na Dr.Hetal Anthan akishuhudia kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Bi Jane Matinde.
Mmoja wa washindi wa shindano la Mkali Nani linaloendeshwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Bw Daniel Mshana(katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja baada ya kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya kwanzaya promosheni ya nani mkali. Pichani (kushoto)ni mshindi Bw Albogast Oiso (kulia) ni Afisa mawasiliano wa Airtel Bi.Dangio Kaniki akifatiwa na moja ya mshindi Dr.Hetal Anthan
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewazawadia washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo washindi wa kila siku wamekabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi wa wiki ameondoka na shilingi milioni tatu.
washindi hao wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Mwanza, Tanga, Mbeya, Arusha na Dar es Saalam
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.
Na leo napenda kuchukua fulsa hii kuwatangaza washindi wa wiki ya kwanza ambao ni Bw Daniel Mshana , Dr. Hetal Anthan na Albogast Oiso wa Dar es saalam, wengine ni Said Seif wa Mwanza,Junior Pesambili wa Arusha na Abdi Ibrahim Mohamed wa Muheza Tanga hawa walijishindia million moja kila mmoja na ambapo bwana Abdi Ibrahim zaidi ya kuwa mshinidi wa siku ameibuka kuwa mshindi wa wiki na kuondoka na pesa taslim shilling million tatu”.
Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde
kujiunga na “Nani Mkali”, mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.
No comments:
Post a Comment