HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 12, 2012

wengi wajitokeza kimzika mzee Kipara leo

Baadhi ya waumini wa Kiislam walifanya idada ya kusalia maiti ya Marehemu Mzee Said Fundi maarufu kwa jina la Mzee Kipara aliyefariki dunia jana Maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Na Francis Dande.

Maelfu ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam na vitongoji vyake, leo wamejitokeza katika mazishi ya msaanii mkongwe wa sanaa ya maigizo, Fundi Said maaruku kama mzee Kipara.

Mazishi hayo yalimenyika jioni hii katika makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Waziri wa Afrika Mashariki, Mh. Samuel Sitta na viongozi wengine akiwemo mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemens pamoja na wasanii mbalimbali.

Mzee Kipara alianza sanaa mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani kabla ya kujiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa ikiitwa TBC Taifa na kukiendeleza kipaji chake alichokuwa amejaaliwa na Mungu ambapo aliweza kuonyesha umahiri katika uigizaji ambao ulimpatia umaarufu mkubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Akiwa RTD Mzee Kipara aliigiza katika michezo mingi na kipengele kilichompatia umaarufu zaidi ni ule uigizaji wake wa kujifanya mbabe na mkorofi na kujikuta akijizolea mashabiki lukuki hasa ukizingatia wakati huo Tanzania ilikuwa na kituo kimoja cha redio na mamilioni ya wanachi walikuwa wakiitegemea kwa ajili ya kupata habari mbalimbali na burudani ikiwemo michezo mbalimbali ya uigizaji iliyokuwa ikirushwa wakati huo.
Baadhi ya Wasafii na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Mzee Kipara wakati wa kuelekea Makaburi ya Kigogo Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Sehemu ya Umati uliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara ukielekea yalipo Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Mpiga Picha wa Globu ya Jamii,Francis Dande akiwa na Muigizaji wa Sanaa ya Maigizo wa siku nyingi,Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small walipokutana kwenye maziko ya Marehemu Mzee Kipara kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad