HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 20, 2012

SPIDER YAWANUFAISHA WATANZANIA KATIKA NYANJA ZA UTAMADUNI, AFYA, VITA DHIDI YA RUSHWA NA HAKI ZA BINADAMU

Na Mdau Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa

Progaramu ya Kiswidishi ya ICT katika nchi zinazoendelea ambayo inaratibiwa na Idara ya Komputa ya Chuo kikuu cha Stockholm Sweden (Spider) kwa kupitia miradi inayoifadhili imeonesha mafanikio makubwa ya  kuwasaidia wananchi wa Tanzania kwenye nyanja za Utamaduni, Afya, Mapambano dhidi ya Rushwa na Haki za Binadamu.

Mafanikio hayo yamejionesha pale viongozi wa miradi inayo fadhiliwa na SPIDER ealiypowasilisha taarifa zao katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na SPIDER. Mkutano uliofanyoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa Miradi iliyofadhiliwa na SPIDER na wadau wa kutoka kwenye taafisi na Vyuo Vikuu nchini.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Dkt Paul Msemwa alisema kuwa, kwa kupitia mradi uliofadhiliwa na SPIDER Watanzania wenye vipaji vya muziki na walio kosa fursa ya kurekodi muziki wao sasa wataipata nafasi hiyo. Aidha watoto watapata nafasi ya kujifunza upigaji wa picha na uhifadhi wake kwa kutumia vifaa vya kisasa.Aidha matukio muhimu yanayothaminiwa na jamii ya kufanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni yatawekewa kumbukumbu na kuhifadhiwa.

Naye Bw Wilfred Warioba Kutoka tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, amesema kuwa kupitia Mradi Uliofadhiliwa na SPIDER wameweza kufanya utafiti wa namna gani wananchi wataweza kutumia njia ya ujumbe wa simu za mkononi kutuma malalamiko yao mbele ya tume na kupata mrejesho. Bwana Warioba aliongeza kuwa Tume inaandaa namba maalum kwa ajili ya zoezi hilo.

Meneja wa Mradi wa e-RCH for Better Care(Huduma Bora ya Uzazi wa 
Mama,Baba na Mtoto kwa kutumia TEHAMA) Bw Jacob Malitinywa amesema kwa kupitia ufadhili wa SPIDER wameza kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuhudhuria Clinic na umuhimu wa kufuatilia afya ya mama, Baba na motto. Wananchi wa Wilaya ya Rufiji ambako mradi unafadhiliwa wameitikia vyema na  mahusiano kati ya vituo vya Afya binafsi na vya serikali yameimarishwa.

Kiongozi wa JUA ARTS FOUNDATION Bw Vitalis Maembe amesema, Mradi wake umeweza kuendesha Kampeni ijulikanayo kama Chanjo dhidi ya RUSHWA, UVIVU na UBINAFSI katika  Mikoa mbali mbali ya Tanzania. Kupitia kampeni hiyo wameweza kufikisha ujumbe na mafunzo kwa wanachi juu ya Ubaya wa Rushwa na namana ya Kupambana nayo, na kusema kuwa wanaendelea kusambaza Chanjo hiyo kwenye mikoa iliyobaki ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kupata elimu hiyo.

Akiwapongeza kwa kazi nzuri iliyo fanywa viongozi wa miradi Mkurugenzi wa SPIDER Dkt Paula Uimonen ameahidi SPIDER itaendelea kushirikiana na Tanzania hasa kwa kupitia miradi inayo ifadhili, na kusisitiza ufadhii huu uwalenge zaidi watanzania ambao wamekuwa wa kikosa fursa zinazo endeshwa na miradi hiyo.

Bw Theophilus Mlaki Mratibu wa Miradi iliyofadhiliwa na SPIDER hapa nchini na mwenyekiti wa mkutano huo, ameushukuru Uongozi wa SPIDER na Serikali ya Sweden kwa kuwa na upendo na imani ya kuisaidia Tanzania katika matumizi ya ICT kwa maendeleo.

Huu ni mkutano wa pili wa SPIDER kufanyika hapa nchini ambapo mkunano wa kwanza ulifanyika mwaka 2011, Programu hii ya SPIDER ya nchini Sweden imefadhili Swedish Krona 2,000,000 sawa na Tsh Milioni 480 kutekeleza miradi  inayo husu ICT na Maendeleo. 
 Meneja wa Mradi wa e- RCH for Better Care Bw Jacob Malitinywa akitoa taarifa za mradi wake uliofadhiliwa na SPIDER.
 Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa akiwasilisha Taarifa za Mradi wa Makumbusho uliodhaminiwa na SPIDER.
 Mkurugenzi wa SIDER Dkt Paula Uimonen akiongea na Viongozi wa Miradi pamoja na Wadau kutoka Vyuo Vikuu nchini katika mkutano wa pili wa SPIDER uliofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
 Kulia ni Mkurugenzi wa SPIDER Dkt Paula Uimonen na Meneja wa Miradi inayofadhiliwa na SPIDER,Tanzania Dkt Katja Sarajeva  wakisikiliza kwa makini Michango toka kwa wadau wa Mkutano.
 Pichani ni Mratibu wa Miradi inayofadhiliwa na SPIDER nchini/Mwenyekiti  Bw Theophilus Mlaki akiongea na wajumbe wa mkutano.
Wajumbe wamkutano wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu Anastasius Liwewa juu ya Studio ya Kurekodi Musiki ambayo ni Moja ya Sehemu ya Mradi Wamakumbusho na Nyumba ya Utamaduni Uliofadhiliwa na SPIDER.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad