Picha inaonesha mtandao wa Wikipedia ukipinga sheria hiyo. |
Kama ulitembelea tovuti kubwa kama Google, Wikipedia na hata Facebook, nadhani uliona kuna ujumbe uliokuwa unaonesha kupinga miswaada miwili ambayo serikali ya marekani inatizamia kuipitisha kuwa sheria. Miswaada hiyo ni SOPA na PIPA.
Lakini unaweza kujiuliza hii SOPA na PIPA ni vitu gani? SOPA ni kifupi cha Stop Online Piracy Act (SOPA) na ile nyingine ya PIPA ni Protect Intellectual Property Act , ni muswaada ya huko marekani ambayo lengo lake ni kukazia zaidi haki miliki kwenye sheria za marekani, kwa sheria hii lengo kubwa ni kulinda wamiliki wa vitu au huduma zinazotolewa online pia kutoa adhabu kali kwa watakaokubwa na kosa hilo.
Kwan sheria hii itampa mamlaka zaidi mmiliki wa haki miliki kuweza kuwasilisha suala lake kwa mapana zaidi huku yakiwaweka kizuizini makampuni au tovuti zote zitakazo vunja sheria hii, iwe ni ya marekani au ya Tanzania.
Swali kuwa ambalo unaweza kujiuliza ni kuwa kwanini wamiliki wengi wa tovuti wameigomea? Je sheria hii haimaanishi kitu kizuri? La hasha, sio kila kitu kizuri lazima kikubaliwe. Kupitishwa kwa sheria hii kutaondoa uhuru wa kujieleza ambao ndio umejenga ulimwengu wa tovuti za leo. Kwa mfano, mtandao wa Facebook na Wikipedia umejengwa kwa misingi ya watu kugawana maarika au taarifa.
Sasa ndani ya sheria hii hutoruhusiwa kugawa taarifa au kumbukumbu ambayo sio yako au bila ruhusa ya mwenye taarifa. Kinyume chake mmiliki wa tovuti atachukuliwa hatua. Hapa tunaenda kwenye kile kitu kilichowafanya Google kutimka Uchina( censorship). Chukulia mfano leo hii unataka kuweka habari kwenye Facebook, ni lazima uhakikishe ile habari ni yako au mmiliki anaruhusu kuiweka kule, la sivyo itakuwa ni kosa.
Wananchi marekani wakipinga sheria hiyo |
Kutokana na maelekezo yaliyomo kwenye sheria hiyo,tovuti zote za marekani zinatakiwa zisifanye biashara wala kuionesha tovuti yoyote ambayo itapatikana na kosa na kwenda kinyume na sheria hii, hii inamaanisha kila tovuti inatakiwa kuwa makini katika mambo mawili
1. Kuangalia kila taarifa wanayoweka haijavunja sheria ya haki miliki(censorship)
2. Kutofanya biashara ya namna yoyote na kampuni yoyote iliyo nje ya Marekani ambayo imeorodheshwa katika wakiukaji wa sheria hii.
Kwa muono wa mbali, hatua hizi ni kuzuia uhuru wa intanet kama wenyewe wanavyouita( Internet Democracy)
Je sisi inatuhusu?
Swali ambalo unaweza kuanza kujiuliza, sheria ya marekani inatuhusu vipi sisi Watanzania? Ukweli ni kuwa sheria hii haitoishia marekani tuu, kwani makampuni ya marekani hayatoruhusiwa kufanya biashara na kampuni yoyote duniani ambayo imevunja sheria ya Marekani na kutofanya hivyo ni kutenda kosa. Pia wasajili wa majina, wahifadhi tovuti(hosting) watatakiwa kuiondoa tovuti yoyote iliyokiuka sheria hii toka kwenye seva zao na mengine mengi. Sheria hii itakuwa na athari kubwa mno kwa mataifa yanayoendelea kama Tanzania ambao hatuna vitu vya kwetu wenyewe.
Hivyo basi, kwa mtazamo wangu naona sheria hii ni changamoto kwetu kujitahidi kuwa na vitu vyetu wenyewe kitu ambacho kitatufanya tuweze kusimama bila shaka kwani kila taifa huleta sheria ambazo zina faida kwao. Ingawa sheria hii imepata upinzani mkubwa toka kwa wamarekani, lakini haukutungwa kwa ajili ya kuwashambulia wamarekani, ni kwa ajili ya mataifa ya nje ila kwakuwa tunaishi katika ulimwengu ulioungannika hivyo kwa njia moja au nyingine wamarekani nao wataathirika. Si unakumbuka waziri mkuu wa uingereza alivyoshikia bango mambo ya jinsia moja na kuzilazimisha nchi zetu kufuata matakwa yake?
Kutokana na sababu hizo, makampuni mengi ya ya intaneti yanaod=na sheria hii ni kama kuwaziba midomo na kuanza kuwa China ya pili.
Je wewe unaonaje??
No comments:
Post a Comment