HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 31, 2012

Airtel yafanya semina kwa Mashirika na sekta mbalimbali nchini kuhusu Airtel Money

Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi kutoka katika makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurungezi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Kalpesh Mehta akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria seminar hiyo iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili katika makao makuu ya Airtel , lengo likiwa ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.
(kushoto) mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor na Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta kwa pamoja wakitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali yaliyoalikwa kupata mafunzo juu ya faida na matumizi ya huduma hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za uendeshaji wa biashara zao. Semina hiyo semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali leo kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari.
Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad