HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2011

ZIARA YA SIKU MOJA YA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI GEORGE W.BUSH TANZANIA

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush (aliekaa kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo.Mh. Bush yupo nchini kwa ziara ya siku moja ambapo leo ametembelea Taasisi ya Saratani katika Hospitali ya Ocean Road,jijini Dar es Salaam akiambatana na Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush akihutubia wakati wa hafla hilo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisikiliza Hotuba hiyo ya Mgeni wake.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akiteta jambo na Mgeni wake Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush wakati wa hafla ya kumkaribisha iliyofanika leo Ikulu,Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush akiwa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati wakitoka Ikulu kuelekea Hospitali ya Ocean Road walikotembelea Taasisi ya Saratani.
Baadhi ya wadau wakipata Taswira wakati wa hafla hiyo.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na aliyekuwa Rais wa Marekani Mh. George W. Bush na mkewe Laura Bush wakizungumza na mmoja wa wagonjwa wa kansa ya funganyonga pindi walipofika kwenye wodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,Jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete na aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush na mkewe Mama Laura Bush wakiwa pamoja na wagonjwa wenye VVU / UKIMWI Sara Daudi, Amina Assenga na Freddy Mwasongola.Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad