HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2011

Mr. Ebbo hatunaye tena,Afariki Dunia usiku wa kuamkia leo

Mr Ebbo enzi za uhai wake.

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa aliyekuwa Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya (bongo fleva),Abel Rusheraa Motika,aliyetambulika na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia jina lake la kisanii la Mr Ebbo amefariki Dunia alfajiri ya leo.

Habari zinaeleza kuwa,Mr Ebbo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake mkoa Tanga na Mipango ya Kusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Jijini Arusha kwa Mazishi inafanywa.

Mr Ebbo wakati wa uhai wake alitamba na kujizolea mashabiki lukuki kipitia vibao vyake kadhaa ukiwemo wimbo wa Mimi Mmasai,Boda Boda,Kamongo na nyingine nyingi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMEN.

2 comments:

  1. Hebu jaribu kuangalia hiyo habari yako vizuri amefariki dunia akiwa wapi Tanga au Arusha? Maana wewe umeendika sehemu zote kafa Tanga mara kafia Arusha hebu rekebisha kidogo tupate habari kamili Mkuu wangu

    ReplyDelete

Post Bottom Ad