HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 2, 2011

Serikali yaitaka TFF kuwaendeleza vijana wa Airtel Rising Stars


Naibu wa Waziri wa Mawasiliano Charles Kitwanga akizungumza na kocha wa shule ya mpira wa klabu ya Manchester United Billy Miller alipotembelea katika mafunzo ya kimataifa ya airtel rising stars kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Mawasiliano  Charles  Kitwanga akisaliamiana na wachezaji wa walioko katika mafunzo ya kimataifa soka inayoendeshwa na makocha wa kutoka shule ya soka ya klabu ya Manchester United.
Kocha wa vijana wa viungo kutoka shule ya soka  ya klabu ya Manchester United Paul Bright akiwatoka wachezaji wa wanaolioko katika mafunzo  ya kimataifa katika mazoezi ya jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SERIKALI  imeIitaka  Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kuhakikisha inawalea vijana  waliopata nafasi ya  kushiriki  kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya ‘ Airtel Rising Stars’ ili waweze kulisaidia taifa hapo baadaye.

Naibu Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa, Charles Kitwanga alitoa kauli hiyo jana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam alipokwenda kuwatembelea washiriki wa kliniki hiyo inayojumuisha mchi za Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.

“Serikali inafurahi kuona mwekezaji kama kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na klabu ya Manchester United ya Uingereza  zimejitokeza kusaidia maendeleo ya soka , hatuna budi kuhakikisha vipaji hivi vinaendelezwa pamoja na kukuza zaidi”, alisema Waziri Kitwanga.

Mheshmiwa Kitwanga alisema,  jukumu la serikali ni kutoa miundombinu inayowezesha michezo kufanyika  hivyo jukumu la kuhakikisha vipaji na elimu wanayoipata vijana hao inabaki kwa taasisi husika akimaanisha TFF.

“Serikali tunaahidi tutaendelea kutoa mazingira mazuri kwa hawa wawekezaji  ili waweze kufanya kazi zao vizuri ili nao waweze kuhamasika na kuweza kusaidia kuwekeza kwenye sekta za michezo kama walivyofanya hawa wenzetu, “ alisema Mheshimiwa Naibu Waziri.

Alisema Tanzania na hata baadhi ya nchi nyingi za Afrika  zimekuwa hazifanyi vizuri sana katika ngazi za kimataifa sio kwasabu hazina vijana wenye vipaji vya soka bali ni kwa sababu hazina program madhubuti  za kuendeleza vijana ambao ndiyo mhimili wa maendeleo ya soka.

Mbali na Naibu waziri huyo, viongozi wengine walioitembelea kambi ya kliniki hiyo jana ni pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile, Osiah, Kocha wa timu ya soka ya Taifa nchini, ‘Taifa Stars’ , Jan Poulsen, Kocha mkuu wa timu za soka za Taifa za vijana nchini, Kim Poulsen, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr  pamojana na viongozi wengine wa Airtel.

Kliniki hiyo iliyozinduliwa na Oktoba 28 na mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Bray Robson inatarajiwa kufungwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad