HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 21, 2011

Watoto wanapofunga mtaa ili kukiendeleza Chandimu

 Kutokana na kukosekana kwa sehemu nyingi za kuchezea watoto ndani ya jiji la Dar,Watoto hawa wakazi wa Ilala Bungoni waliamua kuufunga mtaa wao kwa kuweka magoli huku na kule ili kuendeleza mchezo wao wa mpira wa miguu maarufu kama Chandimu.
 Ambapo ikitokea kuna gari linapita namna hii,basi gemu linasimama kwa muda ili kupisha chombo hicho kipite na baadae kuendelea kama kawa.
 Raha ya mchezo huu siku zote ni magoli,na hapa wakishangilia baada ya upande mmoja wa timu hizo kuufunga ule mwingine.
Gemu linaendelea bila zengwe.
 Hapa zengwe limetokea na kupelekea mwenye mpira wake kuamua kuuchukua mpira huo na kutaka kuondoka baada ya kutakiwa  kutoke pindi alipo kufungisha goli.(Utoto raha jamani,wangapi wanakumbuka haya??)
 Gemu limesimama kwa muda kupisha pikipiki ipite.
Gemu linasonga kama kawa.

1 comment:

  1. Kaka Othman wanifurahisha sana kwa kunikumbusha nyumbani Tanga kila niangaliapo blog yako safi sana, mdau wa Norway.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad