Naibu Waziri wa Viwanda
na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akitazama aina mbali mbali za mboga mboga
katika soko la Tandale.
Naibu Waziri wa Viwanda
na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akitazama aina mbali mbali za maharage
na kunde katika soko la Tandale alipotembelea soko hilo kujionea
hali ya soko na upatikanaji wa vyakula na bei.
Wateja wa mboga mboga wakiwemo
wageni kama walivyokutwa sokoni Tandale wakijipatia bidhaa mbali mbali
za vyakula sokoni hapo.
Wafanyabiashara wa nguo
za mitumba katika soko la Tandale wakizungumza na Naibu Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe lazaro Nyalandu sokoni hapo. Wamemuomba Mh Nyalandu
kuwasaidia kuboresha mazingira ya soko hilo ili kuvutia wateja zaidi.
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Mh Lazaro Nyalandu, amewataka wafanyabiashara na mamlaka husika
kushirikiana ili kuhakikisha kuwa bidhaa katika masoko hazuizwi
kwa bei aghali kuliko bei iliyopangwa katika soko.
Mh Nyalandu ametoa wito huo
Jijini Dar es salaam, mara baada ya ziara yake ya ghafla katika soko
la Tandale ambalo ni miongoni mwa masoko yanayopokea kiasi kikubwa cha
chakula kutoka kwa wakulima kote nchini.
Katika ziara yake hiyo, Mhe
Nyalandu amewataka wafanyabiashara kuwa waungwana na wazalendo kwa kuuza
bidhaa mbali mbali hasa vyakula kwa bei nafuu ili wananchi wenye vipato
vya hali chini waweze kumudu.
Hali ya chakula nchini ni nzuri,
nafaka, mbogamboga na matunda vinapatikana kwa wingi. Wakulima wanawauzia
wafanyabiashara kwa bei nzuri na nafuu, natumia nafasi hii kuwaomba
nyinyi wafanyabiashara kuwa wazalendo, tuwajali wateja wetu kwa kuwauzia
bidhaa hizi kwa bei watakayoimudu, mpate faida kidogo na wenzenu wapate
chakula na mahitaji mengine kwa bei nafuu.
Mhe Nyalandu pia ameutaka uongozi
wa soko hilo kubuni mbinu za kisasa za kuliboresha soko hilo liweze
kuvutia wateja zaidi wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha hali ya usafina
kuzingatia kanuni za afya ili kuwalinda walaji dhidi ya magonjwa yanayoweza
kusababishwa na uchafu.
No comments:
Post a Comment