BENDI
inayoendelea kufanya vizuri katika jukwaa la muziki wa dansi nchini
Mapacha Watatu na Bendi Kongwe nchini, Msondo Ngoma zimeandaa shoo
maalum kwa ajili ya kuwasindikiza ndugu zao kundi jipya la Taarab la
Tanzania Modern Taab (T-Moto) ‘Real Madrid’ katika uzinduzi wa kundi
hilo utakaofanyika Oktoba 28 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akizungumza
na Sufianimafoto, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa
tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na
mazungumzo na bendi hizo zitakazowasindikiza katika onyesho hilo la
uzinduzi ambazo zote zimeitikia wito.
Aidha Amini, alisema kuwa uzinduzi wa kundi hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa albam yao kwanza ya inayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea.
kundi
hilo tayari limekwisha kamilisha albam mbili kwa mpigo, ambapo
itakayozinduliwa siku hiyo ya oktoba 28, tayari nyimbo zake zimeshaanza
kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio.
No comments:
Post a Comment