Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Mozambiq, Mama Graca Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Mama Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo kaburi la mwasisi wan chi ya Mozambiq, wakati wa maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo Msumbiji leo.
Askari
wakimuongoza Rais wa Mozambiq, Armando Guebuza, kuelekea kuweka Shada
la maua katika Kaburi la Mwasisi wan chi hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa
Rais wa nchini hiyo, Samora Machel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora
Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19 mjini Maputo Msumbiji.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na
baadhi ya Marais wa nchi za Afrika wakati walipohudhulia katika sherehe
za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa
Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika leo mjini Maputo Msumbiji.
Kingunge
Ngombale Mwilu, akijumuika na wananchi wa nchini Mozambiq, kuelekea
kuweka mashada ya maua katika kaburi la Mwasisi wa nchini hiyo, wakati
wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa rais wan
chi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment