HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 27, 2011

kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini chazinduliwa jijini Mbeya


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini mjini Mbeya.Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango.
Akizindua ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakati alipokuwa akimkaribisha Waziri Mary Nagu alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Kiwira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Mbilinyi akizungumzia Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji jijini Mbeya kutoka Kushoto Mbele ni Mrs Kadyanji na anaefuatia ni Mrs. Yunge na wajasilia mali wengine.
Jengo la TCI Mkoani Mbeya.Picha zote na Mbeya yetu Blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad