HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 19, 2011

IPU yaiambia Umoja wa Mataifa kuwa inataka mgawanyo wa madaraka na siyo wa utajiri tu


 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda leo akichangia wakati wa mjadala kuhusu fedha na mdororo wa uchumi duniani ambapo amezitaka nchi zilizoendelea kutojisahau kwa kudhani kuwa maendeleo ya nchi hizo hayana uhusiano wa moja kwa moja na nchi zinazoendelea. Hivyo mataifa yote yanahitaji kuungana na kufanyakazi pamoja. Kulia kwake ni Kamishna wa Bunge Mhe. Hamadi Rashid Hamadi ambaye alihudhuria kikao hicho.
 Makamu wa Rais wa Kamati ya Bunge la Dunia inayoshughulikia maendeleo endelevu, Fedha na Biashara Mhe. Hamad Rashid Hamad ametaka Umoja wa Mataifa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha mataifa machanga cha kupata uwaklishi ulio sawa katika vyombo vya kutoa maamuzi hasa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vyombo vya fedha (IFM,WB) na kuongeza uwazi katika chombo cha kimataifa cha Biashara (WTO) ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikiwatajirisha matajiri na kuwaumiza wazalishaji wan chi maskini. Mhe Hamadi (kati) akiwa na Mhe. Susan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki amesema kinachotakiwa ni mgawanyo wa madaraka na siyo wa utajiri tu.
 Mhe. Suzan Lyimo na Mhe. Angela Kairuki wakifuatilia majadiliano ya wajibu wa wabunge wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wanawake na watoto ambapo ujumbe wa Tanzania ulielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kutekeleza malengo namba nne na tano ya millennia ikiwa ni pamoja na changamoto zake.
 Kaimu Katibu wa Bunge Bw. John Joel akishauriana na Katibu wa msafara Bw. James Warburg kwenye kikao cha Chama cha Makatibu wa mabunge  wa IPU kabla ya uchuguzi wa Rais wa Chama hicho leo.
 Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdulrahmin Abdi akihutubia Baraza Kuu la IPU na kuitaka dunia iisadie Somalia badala ya kuishia Afrika Mashariki peke yake.
 Viongozi mbalimbali wakiifuatilia hotuba ya Mhe. Abdi kwa makini
 Spika Makinda na Mhe. Hamadi wakibadilishana mawazo na mjumbe wa IPU
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Masha Fortunatus afuatilia mjadala.
Uganda ndiyo itakayoandaa mkutano wa IPU Marchi 2012. Haya ni baadhi tu ya maandalizi ambao wameanza kufanya kwa ajili ya mkutano huo. Vyombo vya muziki wa utamaduni.Picha zote na Prosper Minja-Bunge

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad