HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 19, 2011

Dkt. Julie Makani apokea tuzo kutoka Royal society Pfizer London


Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake

Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya Anaemia kwenye ugonjwa Sickle Cell

Ni matumaini yake kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Watanzania wote Urban Pulse tunapenda kumpongeza DR Makani kwa mafanikio hayo.

Asanteni

Urban Pulse Creative
Dr Julie Makani akitoa machache.
Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba.
Stephen O'Brien ambaye ni Parliamentary Under Secretary of State, International Development akimpongeza Dr Julie Makani
Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mzee Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani.
Dr Julie Makani akiwa na familia yake.
Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo.
Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad