Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdulrahman
Kasembe a.k.a Dulayo D-Timing anatarajia kuwaongoza wasanii wengine kutoa
burudani katika usiku wa wanavyuo ujulikanao kama Bagamoyo Intercolleges
Night.Pamoja na Dulayo kutakuwa na wasanii wengine wa muziki wa asili na muziki
wa disko utakaoporomoshwa na dj Nature Skills.
Kwa mujibu wa bw. Kim Kimenya ,mkurugenzi wa
kampuni ya Kimkev entertainment Dulayo anayetamba na nyimbo ya “twende mchumba”
ataburudisha kwenye usiku huo unaotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe
28.10.2011 kuanzia saa 2:00 usiku katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni
Bagamoyo (Tasuba),ambapo tiketi za tukio hilo zinapatikana kwenye duka maarufu
la nguo za kiume liitwalo Mrimi classic wear liliopo mjini
Bagamoyo.
Kimenya alisema kuwa usiku huo ambao
unafanyika kwa mara ya kwanza mjini Bagamoyo unatarajia kuhudhuriwa na wanavyuo
wasiyopungua 1500 kutoka vyuo vya Bagamoyo na utakuwa usiku wa rangi nyeupe,
ambapo watakaopendeza kwa mavazi ya rangi nyeupe watazawadiwa fedha taslimu
pamoja na kulala kwa usiku mmoja kwenye hoteli maarufu za mjini
Bagamoyo.
Sambamba na zawadi za waliopendeza pia kutakuwa na zawadi kwa
atakayejibu swali la usiku huo ambaye atajipatia fedha taslimu.
Kimenya amewahakikishia wapenda taaluma na
burudani kuwa usiku huu umeandaliwa kwa umakini mkubwa,hivyo wategemee tulizo la
mioyo yao kwa kuwa kwenye mikono salama ya waandaji na kupata burudani ya
kihistoria katika mji wa Bagamoyo.
Usiku wa Bagamoyo intercolleges night ni
usiku wa taaluma na burudani wenye lengo la kuwaunganisha na kuwaburudisha
wanavyuo wa mji wa Bagamoyo na nje ya Bagamoyo.Pamoja na burudani wanavyuo
watapata nafasi ya kuelezea na kujadili juu ya umuhimu wa kozi wanazojifunza kwa
jamii.
No comments:
Post a Comment