Afisa
Mazingira wa Airtel Tanzania,Manyama Mkama (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani wa sh. mil. 3 kwa Katibu Mkuu wa SHIMIWI,Ramadhan Sululu (wa pili kulia) ikiwa ni sehemu ya udhamini katika michezo ya SHIMIWI itakayofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Tanga.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa SHIMIWI,Moshi Makuka na wa pili kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jane Matinde.
Kampuni ya simu
za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco
Company (TLTC) leo zimetangaza dhamira yao katika kutunza mazingira kwa
kuchangia na kushiriki zoezi la kupanda miti mkoani Tanga.
Tukio hili la kupanda
miti litakafanyika mwanzoni mwa mwezi Novemba kama sehemu ya ufunguzi wa
michezo ya SHIMIWI itakayofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Tanga.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Afisa
Mazingira wa Airtel Tanzania Bwana Manyama Mkama alisema “Airtel Tanzania
kwa kushirikiana na TLTC tutapanda miti zaidi ya elfu tatu katika
shule ya sekondari ya ufundi Tanga na shule ya sekondari ya kilimo
Galanosi ikiwa ni katika kuendeleza mchakato uliowezesha miti
mengine zaidi ya elfu tatu kupandwa katika
maeneo ya barabara ya Sahare, Shule ya Sekondari Kihere, Kombozi, Yusuf
Makamba, pamoja na Shule ya Msingi Msamaweni na TLTC mwaka jana.
Pamoja na kupanda miti Airtel Tanzania tunadhamini
mashindano haya na kutoa kiasi cha shilling milion tatu kama ikiwa ni udhamini
wetu pia kufanikisha mashindano ya SHIMIWI
Hii ni moja kati ya jitihada tulizonazo katika kutambua
umuhimu wa mazingira na kuyatunza.
Airtel na TLTC tumejiunga na waandaaji wa mashindano ya
SHIMIWI kukamilisha jitihada hizi baada ya kutathmini mchanganuo wao
ulioainisha kupambana na changamoto mbalimbali zinazokumba jamii na nchi kwa
ujumla zikiwemo kumomonyoka kwa udongo, kuongezeka kwa gesi ya ukaa
inayopelekea kuongezeka kwa joto kwenye uso wa dunia na nyingine nyingi ambapo
hupelekea nchi kuwa na uhaba wa chakula na maji.
Airtel Tanzania imekua ikichangia sekta mbalimbali ikiwemo
elimu kwa kugawa vitabu mashuleni, kuinua michezo nchini, kuboresha mawasiliano
hasa vijijini na katika mradi huu, imejikita kutunza mazingira kwa kupanda miti
mkoani Tanga. Ni imani yetu kuwa Airtel na TLTC tumechukua hatua sahihi
kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa kushirikiana na SHIMIWI mwaka huu
kupanda miti mkoani Tanga.
TLTC ni wadau washiriki katika mipango mbalimbali ya
kutunza misitu Tanzania ikishirikiana na wazalishaji wa tumbaku katika mikoa
yote. TLTC tumelenga katika kuwaelemisha na kutoa mafunzo kwa wakulima katika
kupanda vitalu na kutengeneza mashamba ya miti, kwa vile miti ni sehemu ya
uzalishaji wa tobacco TLT inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikiksha
inaimarisha uzalishaji bora wa bei nafuu na uunguzaji yakinifu.
Hadi ifikapo
mwaka 2020 TLTC inadhamiria kuwa imefikia kiwango kikubwa cha upandaji wa
vitalu vitakavyo wasaidia wakulima wa tobacco kuacha kutegemea rasilimali ya
misiti iliyopo sasa.
No comments:
Post a Comment