Meneja Masoko wa Kampuni ya kuuza Magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kutangaza gari atakalokabidhiwa Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011,iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu kampuni hiyo yaliyopo Barabara ya Nyerere Rd,jijini Dar.katikati ni Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania, George Rwehumbiza pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors,Alfred Minja (kushoto) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza (katikati) wakifunua gari aina ya JEEP PATRIOT lenye thamani ya shilingi milioni 72 ambalo litakabidhiwa kwa Mrembo atakaenyakua taji la Vodacom Miss Tanzania 2011.kulia ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuuza magari ya CFAO Motors,Alfred Minja (katikati) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania,George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za gari lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya atakayokabidhiwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.
Warembo wakilifurahia gari hilo huku wengine wakilikagua.
No comments:
Post a Comment