Mh. Zitto Kabwe. |
Ndugu zangu wanawavuti salam kwenu, naomba mnifikishie ujumbe huu kwa watanzania. Shukrani zangu za dhati.
(Nimeandika
makala haya nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa
Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia
zangu ziwe as raw as possible -Zitto Zitto and not Zitto a politician).
Jana
asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za
kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu
2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama
mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba.
Habari
hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa
Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii. Habari
zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari
nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze
kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.
Habari
zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa
Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma
kuhusu msiba huu.
Watanzania
waliokuwa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira
sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii.
Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa
kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na
hata ngoma za asili. 'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu
inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu
aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki.
Mpaka
jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa
wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa. Binafsi nilipotembelea
Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla,
akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa.
Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni.
Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika
kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa. Napenda kuwapongeza sana
waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa
mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu
wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa.
Kwa
kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika
juhudi za uokoaji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada,
ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais
aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki.
Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza
siku 3 za kuomboleza. Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona
hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo.
Wangepata
hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao
miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano
hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea
marehemu wetu. Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima,
sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao
japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa
kutojali msiba huu kwa Taifa.
Misiba
huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa
Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio
hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa
Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!
Jumla
ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya
jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV
Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12.
Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria. Natumai mara baada ya kumaliza
maombolezo
haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa.
Mkuu
wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu
Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika
wenyewe kwa kujiuzulu.
Kufukuzwa
kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa
hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.
Mwenyezimungu
atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho
za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi
wetu.
Zitto Kabwe.
ajali hii ni kama ya mv bukoba kila kitu mpaka sasa kwa jinsi sababu za ajali zinavyoelekea kuwa,hivi na baada ya wiki mbili kila kiyu kitasahaulika na meli zitaanza kujaza tena abiria na mizigo mpaka ajali nyingine itakapotokea ndo tunashtuka kwa wiki mbili halafu tunaendelea kama kawaida na mbaya zaidi na barabarani vilevile, kwanini tusiwajibike kila siku ili kuzuia majanga haya kuserve hela,human resources,tunapoteza man power na maendeleo yatatoka wapi bado na wezi waibe hapohapo tena na kila mtu anaona,waliosababisha wafukuzwe wapewe kazi wanaoweza kuwajibika
ReplyDeleteNDUGU ZITTO SHUKRANI KWA MAELEZO YAKO HAKIKA KITU KINACHINISIKITISA SANA NI KUWA MISIBA KAMA HII INATOKEA MARA NYINGI KWENYE VYOMBO WA USAFIRI NA HAKIKI NASHUKURU MARA NYINGI HUTUMA RAMBI RAMBI YAANI HAKIKA NDUGU WATANZANIA NAOMBA RADHI KAMA NTAKOSEA HIZI RAMBI RAMBI ZIMUKUWA KAMA WIMBO USIOKUWA NA UZITO CHA MSINGI MIMI NAFIKIRI JUKUMU LA RAIA NA SERIKALI KUKOMESHA AJALI HIZI ZA MABASI, MELI NAKADHALIKA ZIKOME. KUNA NJIA MBILI MIMI NAONA MOJA WANANCHI KUWA WATU WAKUFAHAMU KUWA MELI A BASI NI LIMEJAA AU BOVU NA KUTOPANDA PILI SERIKALI IDHIBITI KWA VITENDO NA UPENDO RUSHWA KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI NA HOSPITALI MADAWA NA TIBA SEHEMU HIZI NI MUHIMU KWA WANANCHI KUWA SALAMA. NAIMANI MARA HII RAISI NA WANANCHI WATAUNGANA KUPIGA VITI JAMBO HILI. WASALAMU MOHAMMED NASSER NIKIWA ABU DHABI
ReplyDelete