Uongozi na wadau wote wa 'gazeti' mtandao la THEHABARI.COM
unaungana na Watanzania wote katika maombolezo ya ajali na msiba mkubwa
uliotokea Zanzibar, baada ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islander juzi
usiku.
Thehabari imepokea kwa masikitiko makubwa na inawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapone haraka ili warudi kuendelea na shughuli mbambali za ujenzi wa taifa.
Kwa wafiwa tunawaombea kwa Mungu
wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu kwao na taifa.
Mungu awapokee na kusamehewa dhabi zao ili baadaye waingie katika
ufalme wa mbingu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Imetolewa na Mhariri Mkuu wa Thehabari Tanzania, Joachim E. Mushi

No comments:
Post a Comment