Jumuiya
ya wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha kimataifa cha
Kimarekani (USIU) jijini Nairobi; Nchini Kenya imepokea kwa simanzi zito
na masikitiko makubwa habari ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander
Alfajiri ya tarehe 10 Septemba, 2011 ikiwa safarini kutokea Kisiwani
Pemba kuelekea Kisiwani Unguja. Hakika ni janga zito kwa Taifa letu kwa
ujumla.
Jumuiya
ya wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha
Kimarekani (USIU) jijini Nairobi nchini Kenya inapenda kuwasilisha
salamu zetu za dhati kabisa za rambirambi kwa Mheshimiwa Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Ali
Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Viongozi wote
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla, Ndugu zetu wote
waliopoteza Ndugu, Jamaa, Rafiki, Mzazi, Mwenza na kadhalika. Tunamuomba
Mola atupe Moyo wa Ustahimilivu na Imani ya kuweza kupita katika
kipindi hiki kigumu kwetu sote.
Tunamuomba
Mola aliye mwingi wa rehema awalaze Ndugu zetu mahala pema peponi. Pia,
tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii ya kusikitisha waweze pona
haraka na kurejea katika shughuli za kujenga taifa. Amin.
Inna Lillahi wa Inna Illahi Rajuun.
Glen S. Kapya
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania
Chuo cha Kimataifa cha Kimarekani (USIU)- Afrika

No comments:
Post a Comment