Hakika ni msiba mkubwa na pigo kwa kuwapoteza ndugu zetu wapatao 197 na wengine kujeruhiwa
Mpituli Blog inatoa salam za rambirambi kwa wahanga wote waliopata msiba huu mzito,Pia tunatoa salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Jakaya Mrisho Kikwete.Pia salam za pole zimfikie Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh Mohammed Shein.
Bila kuwasahau wale waliojitolea kwenye uwokozi mmeonyesha moyo wa dhati wa upendo.Hakika mmefanya kazi kubwa sana na mwenyezi mungu atawalipa kwa ujumla INSHALLAH.
Timu nzima ya mpituli pamoja na ngwamba lao tunaungana na Watanzania wenzetu kokote pale duniani,Tunaungana nanyi kwa maombolezo pamoja na dua za kuwaombea ndugu zetu walipoteza maisha Mwenyezi mungu awasamehe makosa yao na awalaze mahali pema peponi na kuwaponyesha wale wote walio jeruhiwa wapone haraka na warudi kwenye shughuli zao za kawaida inshallah
AMINI
No comments:
Post a Comment