Ndugu zetu Watanzania,
Kwa
niaba ya Watanzania na wananchi wote wa Afrika Mashariki waishio hapa
Montreal- Canada, tumezipokea kwa majonzi na mshtuko mkubwa taarifa za
ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spicer jana usiku, tarehe 10/9/2011
iliyosabababisha vifo vingi vya Watanzania wenzetu kutoka Zanzibar.
Kwa niaba ya Uongozi wa Montreal Tanzanians Association (http://www.montrealtanzanians.com/),
tunapenda kutoa salamu zetu za rambirambi kwa wananchi wote wa
Zanzibar na Pemba na Tanzania kwa ujumla waliopoteza ndugu, jamaa na
marafiki zao wapendwa katika kindi hiki kigumu cha maombolezo.
Na
pia tungependa kuwapa pole wote waliokoka kwenye ajali hiyo ya
kusikitisha na tunawaombea kwa M/Mungu awapuguzie maumivu na awape
nguvu na faraja.
Mwisho
kabisa, Montreal Tanzania Association (MTA) ingependa kutoa shukrani na
pongezi za dhati kwa wote walioshiriki katika harakati za kuokoa maisha
ya wahanga wa ajali hii na pia katika shughuli za kuopoa maiti.
Tunamuomba Mwenyezimungu aziweke mahali pema peponi nafsi za wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hii.
Ameen.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Uongozi,
No comments:
Post a Comment