Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa siku
tatu unaojumuisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na
Makondrasi uliofanyika leo Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Rais Dr. Jakaya Kikwete (wapili kushoto) akimkabidhi Cheti,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau (wa pili kulia) kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dr. John Magufuli.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau (kulia) akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa Cheti na Rais Kikwete ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau pamoja na wadau wengine wakifatilia mkutano huo.

Picha ya Pamoja.
Na Alfred Ngotezi
Rais
Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango
mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Rais
Kikwete ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu
uliojumlisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi
alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza
tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe
walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.
Akiongea
kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini
Dar es Salaam, Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo,
Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge
pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Katika
siku za karibuni NSSF imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya
miradi hiyo ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es
Salaam na Zanzibar na nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni
NSSF itaanza kujenga Daraja la Kigamboni.
No comments:
Post a Comment