HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 10, 2011

picha za matukio katika ajali ya kuzama kwa meli ya mv Spise Ireland huko Nungwi kaskazini unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wnaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA NAIBU KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEKHE KHAMIS HAJI KHAMIS WAKITOKA NDANI YA HEMA MAALUM LILILOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA KWA AJILI YA KUPOKELEA MAITI ZA AJARI YA MV.SPICE ISLANDERS ILIYOKUWA IKITOKEA UNGUJA KWENDA PEMBA USIKU WA KUAMKIA LEO.
BALOZI SEIF ALI IDDI AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIWA WA KUFUATWA KWA WATU WATAKAOKUJA KUANGALIA MAITI ZAO NDANI YA HEMA, HADI MUDA HUU TAYARI MAITI MBILI ZIMESHA HIFADHIWA NDANI YA HEMA ILO TAYARI KWA KUTAMBULIWA KATIKA MAANDALIZI HAYO IDARA YA MAAFA WAKISHIRIKIANA NA OFISI YA MUFTI WA ZANZIBAR WATAZIHUDUMIA MAITI ZOTE KWA KUZIKOSHA,KUZIVIKA SANDA NA KUZIKA
WATU WALIOJAZANA KUANZIA UWANJA WA MAISARA HADI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WAKISUBIRI KUWATAMBUA MAITI ZAO,KARIBU MATAYARISHO YOTE YANAYO STAIKI KUFANYIWA MAITI YAMEKAMILIKA KINACHOSUBILIWA NI UPOKEAJI WA MAITI, TAYARI WATU WASIOPUNGUA 300 WAMEOKOLEWA WAKIWA WAZIMA WENGI WAO NI WATOTO NA KINAMAMA.

3 comments:

  1. Watanzania tuukubali msiba wetu,tuwape pole wwlionusurika na tuwaombee dua mwenyezi Mungu awaweke pema peponi mabo wametutangulia mbele ya haki kutokana na ajali hii.Pia huu ni wakati wa kuomba vyombo husika vya serikali visilete mchezo na maisha ya watu wahakikishe sheria za usafiri zinafatwa kikamilifu,wasiruhusu kujaza abiria na mizigo kupita kiwango na vyombo viwe katika hali ya ufanyajÅŸ kazi mzuri(seaworth)

    ReplyDelete
  2. kwanza ni toe pole kwa wale wote waliofikwa na msiba na fikiri wakati sasa kwa serikali kuangalia usalama wa vyombo vya majini
    hasa uzidishaji wa abiria.hili nafikiri ni swala la msingi,wananoangalia usalama wangekuwa makini haya yote yasingetokea.polenisana ndugu zetu mliofikwa na msiba huu.
    (activist joachim laiser)

    ReplyDelete

Post Bottom Ad