Hivi ndivyo hali halisi ilivyo katika barabara ya Same - Mombo ambayo imetawaliwa kwa mashimozz makubwa makubwa kama ionekanavyo pichani.
Kama gari lako ni kimeo basi waweza malizia safari yako katika maeneo haya.
Unaona kitu hiki??
Moja ya Basi la Abiria likilazimika kupita pembeni mwa barabara hiyo ili kuyakwepa mashimozz hayo.
Lori likiwa limekula mweleka baada ya kukosa balansi wakati akiyakwepa mashimozz hayo.kama ilivyo ada kwamba mjumbe siku zote huwa hauwawigi na ndio maana nimewafikishia ujumbe huu wahusika,sasa kazi ni kwao.
Sio kwamba wahusika hawaoni mambo haya,ila wako busy wanachonga line za mikopo,kuuziana nyumba za serikali na ziara za mikoani na nje wapate allowance.Tukana CCM saa nane ya usiku watapewa habari nchi nzima muda si mrefu lakini mambo kama ya barabara,shule.umeme,maji nk hayapo kwenye kipaumbele chao.Aibu au tuwaite Waingereza baada ya miaka 50 waje watujengee?
ReplyDelete