Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari na wadau mbalimbali kuhusu mwelekeo wa mvua za vuli za mwezi Oktoba – Desemba 2011 leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema maeneo mengi ya nchi yatapata mvua za wastani na juu ya wastani na kutoa tahadhari kwa wafugaji, wakulima, sekta ya afya na mamlaka za miji nchini kuzibua mitaro ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia taarifa ya mwelekeo wa Hali ya hewa iliyotolewa na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi(hayupo pichani) leo jijini Dare Salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Na. ESTHER MUZE - MAELEZO.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini imesema mvua za vuli katika maeneo
mbalimbali zinatarajia kuanza mwezi Oktoba huku maeneo ya kanda ya ziwa
yakitarajia kupata mvua zaidi ya juu ya wastani.
Akizungumza
na waandishi wa habari na wadau mbalimbali juu ya mwelekeo wa mvua kwa
kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2011 leo jijini Dar es salaam,
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes
Kijazi amesema mvua hizo zitasababisha upatikanaji wa maji nchini
kuongezeka na kusababisha ongezeko dogo la kina cha maji katika mabwawa
ya maji nchini.
Amesema
katika maeneo ya kaskazini ya nchi mvua zinatarajiwa kuanza
katika wiki ya pili ya mwezi Septemba na kuendelea kusambaa
katika maeneo mengine yanayopata mvua misimu miwili kwa
mwaka hasa maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria yakihusisha mikoa ya
kagera , Mara, Mwanza, Shinyanga na kigoma kaskazini.
Ameongeza
kuwa ukanda wa Pwani ya Kaskazini Mikoa ya pwani , Dar-es-
Salaam, Tanga, Morogoro, kaskazini-mashariki , Visiwa Vya Unguja
na Pemba mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Oktoba
ambapo maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki yanayohusisha
mikoa ya Kilimanjaro , Arusha, na Manyara Mvua zinatarajiwa
kuanza wiki ya tatu ya mwezi oktoba 2011 na kuwa za wastani
hadi juu ya wastani.
Aidha
ametoa tahadhari kwa mamlaka mbalimbali za miji zinazohusika na
sekta ya afya kuchukua tahadhari kuytokana na kuwepo kwa uwezekano
wa kutokea magonjwa ya mlipuko sanjari na uzibuaji wa mitaro
inayopitisha maji machafu ili kuepuka mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Kwa
upande wa shughuli za kilimo na mifugo ametoa wito kwa wananchi
kuzingatia ushauri wa maafisa ugani na mifugo walio katika maeneo yao
ili wafaidike na mvua hizo.
Hata
hivyo amesema kuwa upatikanaji wa maji na nishati kwa ajili
ya mifugo wanyama pori na matumizi mengine katika shughuli za
kiuchumi na kijamii yanatarajiwa kuwa wa kutosheleza katka maeneo
mengi.
No comments:
Post a Comment