HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 16, 2011

Moto ulivyoliteketeza soko la Mwanjelwa Mbeya leo



Soko la mwanjelwa linavyoteketea kwa moto eneo la sido jijini mbeya,chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijajulikana
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
Baadhi ya  mabanda sokoni hapo tayari yameteketea kabisa na moto
Kama kawaida kikosi cha maigizo cha zimamoto mbeya kimeendeleza libeneke la maigizo yake ya kwenda kwenye tukio na gari bovu ambalo hata maji ya kuzimia moto huo halina.na hapa wanaonekana askari wa kikosi hicho wakibishana huku moto ukiendelea 
Kufa kufaana....... kibaka tayari ameshaiba na huyooo anatimka zake.
Dada nae hayuko nyuma katika la kujisevia bidhaa sokoni hapo, keshachukua kapeti na kutokomea nalo.
Umati wa watu ukiwa unaangalia soko linavyoteketea
Mama huyu akilia kwa uchungu akiangalia duka lake likiteketea kwa moto
Hii ni hatari.picha na Mbeya Yetu Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad