HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 10, 2011

MICHEZO YA SHIMIWI YAZINDULIWA RASMI JIJI DAR

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi akizungumza na watumishi wa umma leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bonanza la kuanza rasmi kwa maandalizi ya michezo ya SHIMIWI ambayo kitaifa itafanyika mwezi Novemba 2011 jijini Tanga na kuwataka watumishi hao kutenga muda wa kufanya mazoezi na kuepuka matumizi mabaya ya chakula.
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda(wa kwanza kushoto) kushiriki mazoezi ya pamoja na wafanyakazi mbalimbali wa Wizara, Taasisi, Idara za serikali, Wakala, Mashirika na mamlaka za majiji leo katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akizungumza na wafanyakazi mbalimbali wa Wizara, Taasisi, Idara za serikali, Wakala, Mashirika na mamlaka za majiji wakati wa uzinduzi wa Bonanza la SHIMIWI katika viwanja vya TCC Chang’ombe leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi akikagua timu ya wasichana ya mpira wa Netiboli ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi kabla ya kuanza kwa mashindano wakati wa Bonanza la michezo ya SHIMIWI leo katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es salaam.
Mwamuzi wa mchezo wa Kamba na mjumbe wa kamati ya utendaji wa michezo ya SHIMIWI taifa Bw. Khalidi Ruvu (Ruvu K) akitazama kwa makini saa yake kabla kupuliza kipenga kuashiria kuanza kwa mchezo huo kati ya timu ya kamba ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Fedha na Uchumi leo jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza la michezo ya SHIMIWI.
Wachezaji wa Timu ya Kamba wanaume kutoka wizara ya Fedha na Uchumi wakiwajibika katika viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Bonanza la michezo ya SHIMIWI.
Watumishi mbalimbali wa umma wakishiriki mazoezi ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara, Taasisi, Idara za serikali, Wakala, Mashirika na mamlaka za majiji leo wakati wa uzinduzi wa Bonanza la michezo ya SHIMIWI katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad