HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 22, 2011

mbunge viti maalum mkoani mbeya ahitimisha ziara yake kwa kutembelea gereza la Ruanda na kutoa msaada


 Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya,Dr. Mary Mwanjelwa akikabidhi Msaada  wa bidhaa mbali mbali kwa Maafisa wa gereza la Ruanda mkoani Mbeya.
Dr Mwanjelwa akiwa na Maafisa mbalimbali wa Gereza la Ruanda nje ya bwalo la Maafisa hao.Picha kwa hisani ya Latest News Tz.

Na mwandishi wetu,Mbeya

Mbunge wa viti maalum wanawake kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa  wa Mbeya Dk Mary Mwanjelwa ametembelea wafungwa katika gereza la Ruanda lililopo jijini Mbeya katika mfululizo wa ziara zake mkoani hapa.

Mheshimiwa Mwanjelwa katika ziara yake kwenye gereza hilo, alitembelea maeneo mbalimbali kama vile sehemu za jiko, malazi pia zahanati ndogo ya gereza hilo ambapo mkuu wa gereza hilo ACP Mbunda alimtembeza maeneo hayo na baadae kuongea na wafungwa hao na kushirikiana chakula katika gereza hilo.

Wakieleza baadhi ya kero gerezani hapo, Mkuu wa gereza ACP  Mbunda alisema baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa mbalimbali ambayo mengine yangeweza kuzungumzika mtaani na wengine kushindwa kupata nakala za hukumu,tangu mwaka 1996 hali ambayo inapelekea kuendelea kuongeza mrundikano wa wafungwa katika gereza hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa viti Maalum Dk Mwanjelwa aliwashukuru askali hao kwa moyo wa uvumilivu kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kuwaasa kuwa serikari inayatambua matatizo yao na kwamba inayafanyia kazi, hivyo wasife moyo kwani serikali inawajali watumishi wake.

Aidha Dk Mwanjelwa aliwaahidi kuwa kero zao atazifikisha sehemu husika na alikubali ombi lao la kupatiwa king'amuzi cha runinga ambacho waliomba katika risala yao iliyosomwa kwake na mmoja wa wafungwa gerezani hapo.

Akihitimisha ziara yake katika gereza hilo Mbunge huyo wa viti maalum mkoani Mbeya, alitoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao yakiwemo mafuta ya kupakaa na  sabuni za kufulia, ambapo mbunge huyo alisema waupokee kwa moyo mmoja msaada huo kama ishara ya upendo kwao kwani magereza sio mahali pa adhabu bali ni mahali pa kurekebisha  mtu tabia ingawa wengine wamefikishwa hapo kwa kuonewa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad