Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia,Mh. Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mama Asha Bilal (kulia) na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilala akisalimiana na Rais wa Malawi,Bingu wa Mutharika walipokutana kwenye Ofisi za Mahakama Kuu mjini Lusaka Zambia jana wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata mjini Lusaka jana.katikati ni Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) na mkewe Mama Asha Bilal (wa pili kushoto), Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa (kushoto) na Rais wa kwanza wa Zambia,Dkt. Keneth Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia.Amour Nassor VPO.
No comments:
Post a Comment