Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi,
Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi
msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria
wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa.
Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri
wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar
anakoishi.
Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara
hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake
wataweza kumsaidia kwa hali na mali.
“Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha,” alisema Kuyunga.
N.B. Kutoa ni moyo na siyo utajiri, hivyo hima popote ulipo nchini,
msaidie mzee huyu kwa kumtumia kiasi chochote utakachojaaliwa kwa njia
ya M-PESA AU TIGO PESA, itamfikia mwenyewe moja kwa moja na unaweza
kuongea nae kwanza. Elfu 2 utakayomtumia ina msaada mkubwa kwake na
Mungu atakulipa - WEB MASTER.


No comments:
Post a Comment