HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 19, 2011

Airtel yachezesha droo ya mwisho ya kwanjuka na mshindi kuibuka na million 20

Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Airtel,Dangio Kaniki akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 50 kwa mshindi wa promosheni ya kwanjuka,Padri Isaya Gowa wa Kanisa la Katoriki,Jimbo la Mahenge,Morogoro.Katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando.
 Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Airtel,Dangio Kaniki akiongea na mmoja wa washindi milioni 1 wa promosheni ya Kwanjuka leo wakati wa kufunga droo ya promosheni hiyo,Kushoto ni Afisa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,Humud Abdulhussein.

Kampuni ya simu za mkoni Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Kwanjuka. Promosehen ya kwanjuka ilikuwa ikiendeshwa na Airtel tangu April 24 2011.

Akizungumza na waandishi wakati wa kucheza droo ya mwisho ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “ Tunachukua fursa hii kuwashukuru washindi wote pamoja na washiriki wa promosheni ya kwanjuka ambao kwa kushiriki kwao ndio mafanikio ya promosheni hii.

Promosheni ya Kwanjuka ilikuwa na lengo la kurudisha kiasi cha faida tunayoipata kwa wateja wetu na ndio maana promosheni hii ilileta mafanikio zaidi na tuliamua kuongeza zawadi na muda wa promosheni ili kuendelea kuwafaidisha wateja wetu zaidi.

Leo hii tunafikia mwisho wa promosheni tukiwa tunahistoria ya kupata washindi kutoka sehemu mbalimabli hasa mikoani, na leo tupo na mshindi wetu wa kwanza wa million 50,Padri Isaya Gowa kutoka Morogoro. 

Droo ya leo tunamtafuta mshindi wa million 20 ambaye tutampata hivi punde na ndipo promosheni yetu itakapokuwa imefikia mwisho. Wanaoingia katika droo hii leo ni wale wateja waliojiunga na kushiriki promosheni ya Kwanjuka, ili kujiunga mteja alitakiwa kutuma neno KWANJUKA kwenda namba 15656 kisha mteja alianza kupokea maswali na akiyajibu kwa usahihi alijiongezea pointi ya kuwa mshindi Bado Airtel tutaendelea kuandaa promosheni kabambe kama hizi na hivi karibuni tegemeeni promosheni kubwa zaidi . 

Vile vile Airtel tunaendelea kuboresha huduma zetumjini na vijijini kwa kuwapatia wateja wetu huduma bora kwa gharama nafuuu kuliko mtandao wowote. Kwa sasa Airtel tumepunguza Gharama za viwango vya kupiga simu Kenya na Uganda na kuwapatia wateja wetu punguzo la kudumu kupiga Airtel Kenya na Airtel Uganda kwa gharama mpya nafuu zaidi ya Sh 2 na senti 50 tu kwa sekunde badala ya Sh 5 na senti 30! 

Pia wakati kampeni yetu ya Hamia Airtel ikiendelea nchi nzima wiki hii tunatarajia kuzindua huduma za mawasiliano huko Kibena Iringa, Lumecha Ruvuma na Kiwira Ikuti Mbeya ambapo tunaendelea kutimiza dhamira yetu ya kufikisha huduma zetu za mawasilino katika miji na vijiji mbalimbali na kuwafikia watanzania wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad