HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 19, 2011

TTCL yaanzisha uhusiano wa kibiashara na kampuni ya Maxcom Africa

 Meneja Masoko wa Maxcom, Vitalis Mruma akiongea leo kwenye makao makuu ya TTCL jijini Dar leo
Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Maxcom, Ahmed Lussasi (shoto) akimkabidhi mashine ya kulipia huduma za Vocha za simu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Said Amir Said kwenye hafla hiyo
Picha na habari na  Francis Dande 
wa  Globu ya Jamii

Kampuni ya Maxcom Africa leo imezindua ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya simu Tanzania (TTCL) ukiwa na lengo la kukuza mahusiano ya kibiashara kati ya kampuni hizo mbili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa Maxcom, Ahmedi Lussasi alisema kuwa kampuni yake ni ya ina zawadi ya mawakala 1300 nchi nzima kati yao zikiwa ni matawi 200 ya shirika la Posta ambapo matarajio ya kampuni hiyo ni kufikia mawakala 2500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

 Aidha alisema kuwa, Maxcom inajishughurisha na utoaji wa huduma za kuuza umeme wa Luku, huduma ya kutuma na kupokea Pesa ya Mpesa, malipo ya ving’amuzi vya televiisheni (Startimes &DSTv) na Uuzaji wa kadi za simu za viganjani za mitandao yote, huduma hizo zinapatika nchi nzima. 

“Kampuni yetu inatoa huduma kama hizi katika nchi ya Rwanda na kupata mafanikio makubwa kuitokana na kutoa huduma bora na zenye uhakika ambapo kwa ushirikiano huu kampuni ya TTCL itaweza kukua kibiashara kutokana na uwezo mkubwa wa usambazaji wa kampuni ya Maxcom Africa’, alisema Meneja wa Maxcom, Lussasi. 

“Napenda kukuhakikishia wewe na kampuni yako kuwa Maxcom imejipanga vizuri na kuboresha na kuongeza bidhaa zaidi ambapo kwa sasa  vocha TTCL zitakuwa zikipatikana kwa urahisi zaidi katika kila kona ya nchi yetu kupitia kwa mawakala wetu Maxcom. 

Naye Ofisa Mtendaji wa TTCL, Said Amir Said alisema kuwa ushirikiano  wa kibiashara walioingia na kampuni ya Maxcom utakuwa chachu katika kufikia malengo ya kibiashara pamoja na kuwafikia wateja wao kwa urahisi zaidi kupitia kampuni hiyo na kuleta ushindani wa kibiashara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad